Genesis 27:37-40

37Isaka akamjibu Esau, “Nimemfanya yeye kuwa bwana juu yako, pia nimewafanya ndugu zako wote kuwa watumishi wake, nimemtegemeza kwa nafaka na divai mpya. Sasa nitaweza kukufanyia nini, mwanangu?”

38Esau akamwambia baba yake, “Je, baba yangu una baraka moja tu? Unibariki mimi pia, baba yangu!” Kisha Esau akalia kwa sauti kubwa.

39Baba yake Isaka akamjibu, akamwambia, “Makao yako yatakuwa
mbali na utajiri wa dunia,
mbali na umande wa mbinguni juu.

40 Utaishi kwa upanga,
nawe utamtumikia ndugu yako,
lakini wakati utakapokuwa umejikomboa,
utatupa nira yake
kutoka shingoni mwako.”

Yakobo Anakimbilia Kwa Labani

Copyright information for SwhKC